WAKALA WA MABASI YAENDAYO HARAKA
Kumb. Na. AB.23/134/01-J/107
04 Juni 2021
TANGAZO LA AJIRA YA MUDA MFUPI
___________
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Mabasi Yaendayo Haraka, anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye
sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi kumi na tano (15) kama ilivyobainishwa
katika tangazo hili.
1. WASIMAMIZI WA MAPATO
WASAIDIZI (REVENUE MANAGEMENT
ASSISTANT) – NAFASI 09
1.1. SIFA
ZA MWOMBAJI:
Awe na Elimu ya kidato cha nne (IV) na amehitimu elimu ya
ngazi ya cheti katika fani za Uhasibu, Biashara,
Manunuzi, Takwimu, Hisabati au nyingine inayofanana na hizo kutoka chuo
kinachotambulika na Serikali.
1.2. MAJUKUMU
YA KAZI:
i.
Kufuatilia utararibu wa utaoaji tiketi kwenye mashine
(TOMs);
ii.
Kuhakikisha abiria wote wana tiketi;
iii. Kuhakikisha
“attendants” wanachana tiketi
zilizotumika; iv. Kuhakikisha tiketi zilizotumika haziuzwi tena kwenye mfumo;
v.
Kushauri juu ya umuhimu au ulazima wa utoaji wa tiketi
nyingi kulingana na uhitaji wa usafiri kwa kituo husika;
vi.
Kuhakikisha kiwango cha makusanyo ya vituo kinaakisi
makusanyo yaliyokabidhiwa kwa wasimamizi wa kazi na kuwasilishwa Benki kwa siku
husika;
vii.
Kutoa taarifa juu ya viashiria vya ubadhilifu na mambo
mengine yasiyo ya kawaida katika ukusanyaji wa nauli; na
viii.
Kufanya kazi nyingine zinazohusiana na usimamizi wa
mapato atakazo pangiwa na msimamizi.
1.3 MSHAHARA:
Kima cha mshahara kwa mwezi ni hadi shilingi
310,000/=.
2.
WAHUDUMU WA ABIRIA – NAFASI 06:
2.1.
SIFA ZA MWOMBAJI:
Awe na elimu ya kidato cha nne na amehitimu elimu ya
ngazi ya cheti katika fani za Afya ya Jamii (Community Health) au fani nyingine
inayofanana na hizo kutoka chuo kinachotambulika na Serikali.
2.2.. MAJUKUMU YA KAZI:
i.
Kuwaelekeza abiria sehemu ya kunawa mikono,
ii.
Kuhakikisha abiria wamenawa kabla ya kuingia katika
usafiri wanaingia katika usafiri,
iii.
Kutoa taarifa ya mahitaji ya vitendea kazi kwa
msimamizi kadiri itakavyohitajika,
iv.
Kusafisha na kujaza maji katika matenki kwa wakati,
v.
Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa
kazi.
2.3.
MSHAHARA:
Kima cha mshahara kwa mwezi ni
hadi shilingi 310,000/= kulingana na mahudhurio.
3.
MASHARITI YA JUMLA:
i.
Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania,
ii.
Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa,
iii. Waombaji
wote wawe na umri usiozidi miaka 45, iv. Waombaji
waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na
namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa
kuaminika,
v.
Maombi yote yaambatane na vyeti vya kidato cha nne,
taaluma, kwa wale waliohitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi
husika waambatanishe vyeti vya mafunzo husika,
vi.
Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of
results”, hati matokeo za kidato cha nne (FORM
IV RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA,
vii.
Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni.
viii.
Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti
vyao vimehakikiwa na Baraza la Mitihani Tanzania –
(NECTA), ix. Uwasilishaji wa taarifa, nyaraka na sifa za kughushi, wahusika
watachukuliwa hatua za kisheria.
Maombi yote yatumwe
kwa njia ya posta kupitia anuani ifuatayo:-
Mtendaji Mkuu,
Wakala Wa
Mabasi Yaendayo Haraka,
S.L.P. 724,
DAR ES SALAAM.
Mwisho wa kupokea
maombi ya kazi ni tarehe 13 Juni 2021.
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa
katika tangazo hili HAYATAKUBALIWA.
Limetolewa na:
MTENDAJI MKUU
WAKALA WA MABASI YAENDAYO HARAKA
No comments:
Post a Comment